Ni mabingwa wa soka la Tanzania kwa msimu wa ligi kuu ya NBC 2022/23, ambao wamekamilisha historia yao katika namna ya kipekee kabisa, kwa kuandaa documentary ambayo imebeba taswira nzima ya timu hiyo kwa mafanikio waliyoyapata katika msimu uliopita, ikiwa ni pamoja na kutwaa mataji matatu ya ndani na kutinga fainali za shirikisho barani Afrika.
Uzinduzi huo umefanyika hapo jana katika ukumbi wa Dar Free Market Mall, huku badhi ya wadau wa michezo wakisema, ‘ilikuwa ni lazima kwa Yanga SC kufanya hivyo kwani msimu bora kama ule si rahisi kujirudia, hivyo ni muhimu kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo”
Documentary hiyo inapatikana katika App ya Azam Max kiganjani mwako kwa bei ya shilingi 2500/= za kitanzania.
#KonceptTvUpdates
#Yangasc