Katika kuendeleza mapambano dhidi ya maendeleo ya nchi, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko kadhaa katika ngazi mbalimbali za mawaziri. Miongoni mwa maeneo muhimu yaliyofanyiwa mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo;
A) Uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu
Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Katika nafasi ya Naibu Waziri Mkuu, atashughulikia Uratibu wa Shughuli za Serikali.
B) Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri
1. Mhe. Jerry William Silaa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
2. Mhe. Anthony Peter Mavunde ameteuliwa kuwa Waziri wa Madini.
3. Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ameteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi.
4. Mhe. Innocent Lugha Bashungwa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.
5. Mhe. Godfrey Msongwe Kasekenya ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.
6. Mhe. Alexander Pastory Mnyeti ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
7. Mhe. David Mwakiposa Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi.
8. Mhe. Judith Salvio Kapinga ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati.
9. Mhe. Dunstan Luka Kitandula ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
C) Uhamisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri
1. Mhe. January Yusuf Makamba amehamishwa kutoka Wizara ya Nishati kwenda kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.
2. Mhe. Stergomena Lawrence Tax amehamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenda kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
3. Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa amehamishwa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
4. Mhe. Angellah Jasmine Kairuki amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwenda kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
5. Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
6. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amehamishwa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
7. Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato amehamishwa kutoka Wizara ya Nishati kwenda kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
D) Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu
1. Prof. Godius Walter Kahyarara ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.
2. Mhandisi Cyprian John Luhemeja ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
3. Balozi Prof. Kennedy Gastorn ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
4. Dkt. Ally Possi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.
5. Bw. Ludovick Nduhiye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi.
6. Mhandisi Mwajuma Juma Waziri ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.
E) Uhamisho wa Makatibu Wakuu
1. Prof. Jamal Adam Katundu amehamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.
2. Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe amehamishwa kutoka Wizara ya Afya kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
3. Dkt. John Anthony Jingu amehamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.
Uteuzi huu unaanza leo, tarehe 30 Agosti, 2023, na viongozi walioteuliwa watapewa kiapo tarehe 1 Septemba, 2023, Ikulu Ndogo, Zanzibar, saa 5:00 Asubuhi. Hatua hizi zinatarajiwa kuimarisha utendaji wa serikali na kuweka msingi imara kwa maendeleo ya taifa la Tanzania.
#KonceptTvUpdates