Akitolea maelezo ya kina kuhusu sakata linaloendelea la mpango wa uwekezaji kati ya Klabu ya Simba na mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio, amesema watu wengi wanazingatia zaidi upande wa Mwekezaji na kusahau kuhusu majukumu ya Klabu ya Simba.
Erio alisema, “Baada ya kukamilisha masharti ya Mwekezaji na ya Simba, tuliutoa cheti kuwa muungano umepitishwa na kile ambacho kilikuwa kinaombwa kimeridhiwa, na sasa kinachofuata ni utekelezaji.”
Aidha, aliongeza, “Wiki mbili zilizopita, upande wa Klabu (Baraza la Wadhamini wa Klabu) walitakiwa kufika RITA (Wakala wa Usajili, Ufilisi, na Udhamini) ili kuhakikisha Hati za Jengo la Klabu zote zinakuwa mali ya Simba Sports Club Limited. Hata hivyo, sina taarifa kamili kuhusu jinsi mambo yalivyosonga mbele kuhusu suala hilo.”
#KonceptTvUpdates
#fcc