DCEA Tanzania yafanikisha operesheni ya siku 8 mkoani Morogoro kwa matokeo mazuri ya kukamata jumla ya gunia 131 za bangi kavu, kilo 120 za mbegu za bangi, na kuteketeza jumla ya hekari 489 za mashamba ya bangi.
Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, DCEA imedhihirisha jitihada zao katika kupambana na biashara haramu ya bangi nchini. Katika wilaya ya Morogoro vijijini, katika Kata ya Kisaki, Kijiji cha Rumba, walifanikiwa kukamata gunia 70 za bangi. Pia, Kijiji cha Mbakana walikamata gunia 59 za bangi na kilo 120 za mbegu za bangi, ambapo mashamba yenye ukubwa wa hekari 350 yaliteketezwa.
Wilayani Mvomero, mamlaka za usalama zilifanikiwa kuteketeza hekari 139 za mashamba ya bangi, na katika wilaya ya Morogoro wakakamata gunia mbili (2) za bangi.
Hii ni hatua muhimu katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya na inathibitisha azma ya Tanzania katika kudumisha usalama na ustawi wa wananchi wake.
#KonceptTvUpdates
#Eastafricatv