Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa ya mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 2 Agosti 2023 Saa 6:01 usiku. Ambapo kwa Mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama ifuatavyo:
Dar es Salaam Petroli ni Tsh. 3, 199, Tanga ni Tsh. 3,245, na Mtwara ni Tsh. 3,271.
Mabadiliko ya Bei za Mafuta mwezi Agosti 2023 yametokana na Changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani, madadiliko ya sera za kikodi, kushuka thamani ya shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, Ongezeko la Gharama za Mafuta.
Hivyo, EWURA imewataka Wafanyabiashara wa bidhaa ya Mafuta ya Petroli kuuza kama bei kikomo zilivyoorodheshwa.
#KonceptTvUpdates