Kufuatia Moto uliozuka katika jengo la ghrofa tano katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini limesababisha vifo vya zaidi ya watu 70 huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Moto huo umetokea katika jengo lililopo katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara la jiji hilo kubwa la Johannesburg.
Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kitengo cha Huduma za Dharura cha jiji la Johannesburg, Robert Mulaudzi, moto huo umesababisha pia watu wengine takriban 52 kujeruhiwa.
Hata hivyo Mulaudzi amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi kwa kuwa jitihada ya kutafuta miili ya watu kutoka ghorofa moja kwenda nyingine inaendelea.
Katika taarifa yake ya ziada aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, kampuni ya awali iliyokuwa ikijulikana kama Twitter, msemaji huyo amesema watu kadhaa wameokolewa.
Jengo lililozuka moto ni makazi holela ya watu licha ya mpaka hivi sasa kutofahamika chanzo cha moto huo.
Pamoja na hiyo, akinukuliwa na vyombo tofauti vya habari nchini Afrika Kusini msemaji huyo amesikika akisema jengo hilo lililowaka moto lilikuwa linafanywa makazi kwa wasio na majumba.
Lakini pia mbali ya vifo vilivyotokana na moto, vipo vya baadhi ya watu ambao wanatajwa kufanya jaribio la kuruka kutoka katika jengo hilo refu,katika nyakati za usiku, kipindi ambacho moto huo unaendelea kwa lengo la kutaka kunusuru uhai wao.
#KonceptTVUpdates