ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, October 3, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

JNIA YASHIKA NAMBA NNE AFRIKA UBORA WA USALAMA

SUZO SHUKRANI by SUZO SHUKRANI
Aug 24, 2023
in HABARI
0
JNIA YASHIKA NAMBA NNE AFRIKA UBORA WA USALAMA
0
SHARES
34
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso ameipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kushika nafasi ya nne barani Afrika kwa ubora wa usalama wa usafiri wa anga kupitia ukaguzi uliofanywa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) kwa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa mwaka 2023.

RelatedPosts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

Oct 2, 2023

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

Oct 2, 2023

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

Oct 2, 2023
Load More

Akizungumza jijini Dodoma mara baada kupokea taarifa ya Uendeshaji wa Viwanja vya ndege nchini Mhe. Kakoso amesema pamoja na huduma bora zinazotolewa katika Kiwanja cha Julius Nyere Interbational Airport, TAA iongeze ubunifu zaidi ili kuvutia mashirika mengi zaidi kutumia kiwanja hicho ili kuchochea uchumi kupitia usafiri wa anga nchini.

“Nawapongeza Serikali kwa kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya viwanja vya ndege kwani matokeo tayari yameanza kujionyesha kupitia kaguzi zinazofanywa na ICAO, hatua hii ionyeshe umuhimu wa kuwekeza zaidi ili mashirika yaongezeke na tuendelee kuaminika zaidi’ Amesema Mhe. Kakoso.

Mhe. Kakoso ameitaka TAA kuhakikishia inaharakisha zoezi la kutafutia hati viwanja vyote nchini ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza kutokana na wananchi kuvamia na kujenga katika maeneo ya viwanja nchini.

Aidha, Mhe Kakoso ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kutenga fedha kwa maeneo ambayo hayana viwanja vya ndege ili kurahisisha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kupitia usafiri wa anga kwani Serikali imeendelea kununua ndege mpya.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha viwanja vyote nchini vinatoa huduma bora na zinazokidhi viwango vilivyowekwa kimataifa kulingana na vigezo vya ICAO.

Naibu Waziri Mwakibete ameongeza kuwa kwa sasa Serikali inaharakisha kukamilisha mradi wa ufungaji taa kwa kiwanja cha ndege cha Dodoma ili kukiwezesha kiwanja hicho kutumika saa 24 ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

#KonceptTVUpdates

Related

SUZO SHUKRANI

SUZO SHUKRANI

Related Posts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10
HABARI

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
HABARI

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM
HABARI

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI
BIASHARA

MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA
HABARI

SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA
HABARI

TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

August 2023
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In