ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 23, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Kamati ya Bunge yatembelea Banda la NMB Nane Nane jijini Mbeya

I am Krantz by I am Krantz
Aug 8, 2023
in HABARI
0
Kamati ya Bunge yatembelea Banda la NMB Nane Nane jijini Mbeya
0
SHARES
22
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

Sep 22, 2023

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

Sep 21, 2023

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

Sep 21, 2023
Load More

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, imetembelea Banda la Benki ya NMB katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika jijini Mbeya, ambako pamoja na mambo mengine ilielezwa Mpango Mkakati wa taasisi hiyo katika kuwawezesha wadau wa Biashara, Kilimo na Mifugo kupitia mikopo ya riba nafuu.

 

Ikiongozwa na Mwenyekiti David Kihenzile ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kusini mkoani Iringa na Makamu Mwenyekiti Mariam Ditopile, kamati hiyo ilielezwa ya kwamba licha ya kuwa NMB imeshatoa mikopo ya zaidi ya Sh. Trilioni 1.61 katika kipindi cha miaka sita, Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ni miongoni mwa Sekta za Kimkakati zinazopewa kipaumbele na NMB, kiasi cha kutengewa bajeti nono kila mwaka.

Meneja Uhusiano wa Kilimo Biashara wa NMB – Kanda ya Nyanda za Juu – Fabian Mnyanyika, aliieleza Kamati hiyo kuwa, licha ya benki yake kuwa ya kwanza kushusha riba ya mikopo ya Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na misitu hadi kufikia asilimia 9 na kukopesha zaidi ya Sh. Trilioni 1.61 katika miaka sita, pia imetenga zaidi ya Sh. Bilioni 40 katika kipindi cha miaka miwili, Bil. 20 kati ya hizo ni kwa ajili ya kukopesha wadau wa Sekta hizo, huku Sh. Bilioni 20 zikiwa ni za mikopo ya ujenzi wa maghala Tanzania nzima.

 

Mnyanyika alibainisha kwamba, kumekuwa na mwitikio mkubwa miongoni mwa wakulima kukopa, ambako tayari wameshakopesha zaidi ya Sh. Bilioni 7 hadi Julai mwaka huu, ikiwemo mikopo inayohusisha pesa taslimu, pamoja na zana za Kilimo, Matrekta, ‘power tiller’ na pembejeo, kutoka Kampuni ya Agricom Africa, washirika wao wa kibiashara katika kuwakomboa wakulima nchini.

 

Akaongeza kuwa, katika msimu wa mavuno, wakulima wamevutiwa na kuchangamkia mikopo ya ujenzi wa maghala ili kukabiliana na upotevu na uharibifu wa mazao, ambako mkopaji anapaswa kuwa na kiwanja kilichopimwa, chenye hati Ili kukidhi matakwa ya kidhamana yaliyowekwa na benki hiyo, sambamba na kuahinisha thamani ya ghala analokusudia kujenga.

 

Mwenyekiti Kihenzile ameipongeza NMB sio tu kwa kuisapoti Serikali katika program ya kuandaa Vijana na Wanawake Kujenga Kesho Iliyo Bora (BBT), bali kwa kutenga mabilioni ya mikopo kwa wadau wa mnyororo huo wa thamani, pamoja na kushusha riba hadi asilimia 9 na kuzingatia nyakati sahihi za mkopaji kufanya marejesho.

 

 

Related

I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy
BIASHARA

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

by I am Krantz
Sep 22, 2023
DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA
HABARI

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA
HABARI

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA
AFYA

MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST
HABARI

SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO
HABARI

TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

August 2023
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In