Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Kituo cha Afya cha mama na mtoto Kizimkazi Dimbani tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi kwa mwaka huu yalizinduliwa rasmi Agosti 26 na shughuli mbalimbali zimeendelea kufanyika kuelekea kilele chake kitakachofanyika Agosti 31.
Rais Samia pia amezindua ukumbi wa mitihani katika shule ya Sekondari Muyuni B, uliojengwa kwa ufadhili wa benki ya Azania, madarasa sita katika Shule ya Msingi Muyuni B, pamoja na kituo cha huduma za mama na mtoto kilichounganishwa na huduma ya M-MAMA inayotolewa na kampuni ya Vodacom.
Pia amefanya ugawaji wa Gari la OCD Kizimkazi Mkunguni pamoja na Gari la OCD Makunduchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan katika muendelezo wa shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi linalofanyika Mkoa wa kusini Unguja.
#KonceptTVUpdates