Wananchi kutoka katika jamii ya kifugaji ya Kimaasai wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamejitokeza kulaani vikali tukio la kushambuliwa kwa Wanahabari waliokuwa wakishiriki kampeni ya kuwahamasisha wakazi wa eneo hilo kuhama kwa hiyari na Kwenda katika maeneo ya Msomera, Kitwai na maeneo mengine yanayowavutia na watakayoyachagua wenyewe.
Wananchi hao wakiongozwa na Viongozi wa Mila na dini kutoka katika Kijiji cha Kapenjiro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, wamefanya Tambiko la kuomba msamaha kwa waandishi waliofanyiwa vitendo hivyo kwa kupigwa na kujeruhiwa na vijana wa kimasai katikati ya mwezi agosti 2023.
Kiongozi wa Kikatoliki Parokia ya Nainokanoka, Katekista Edward Leyani alisema wanawaombea msamaha wale wote waliohusika na tukio hilo kwa kuwa Mungu ndio mpatanishi wa kila jambo na huwa hapendi uvunjifu wa amani katika eneo lolote kwani wote ni watu wake.
Leyani alisema wale wote waliokuwa tayari walifanya maamuzi yao kwa hiari yao na wale wote wanaodai kuwa kuna watu wanawalazimisha wananchi wa Ngorongoro kuhama hiyo sio kweli kwani wanafanya hivyo kwa maslahi yao.
Alisema na kusisitiza kuwa wananchi wa jamii ya kimasai wako tayari kuhama kwa kutii maagizo ya serikali inayoongozwa na Rais Samia na kusema kuwa hawatakubali kurubuniwa na mtu,kikundi kwa maslahi yao kwani maamuzi ya kuhama ni yao wenyewe na sio kulazimishwa.
#KonceptTVUpdates