Waziri wa elimu wa Ufaransa Gabriel Attal amesema mamlaka itapiga marufuku wanafunzi kuvaa abaya wakati wanapokuwa shule.
Vazi la abaya ambalo linachukuliwa kuwa buibui la mtindo wa kisasa huvaliwa na baadhi ya wanawake wa kiislamu kama stara.
Katika mahojiano na shirika la habari la Ufaransa la TF1, waziri huyo ameeleza kuwa atafanya mazungumzo mapema wiki hii na wakuu wa shule za umma ili kuwasaidia kutekeleza marufuku hiyo.
Marufuku hiyo itaanza Septemba 4, 2023 baada ya muhula mpya wa masomo wan chi hiyo kuanza rasmi.
Hatua hiyo inakuja baada ya Ufaransa kupiga marufuku alama za kidini katika shule za serikali na majengo ya serikali, ikisema kwamba zinakiuka sheria za kilimwengu.
Ufaransa imepiga marufuku mavazi au alama zozote za kidini katika shule za umma ikisema inafanya hivyo ili kutenganisha serikali na dini.
Inakadiriwa kuwa, waislamu kati ya milioni 3.5 hadi milioni 6 wanaishi nchini Ufaransa, taifa lenye idadi ya watu wapatao milioni 67.
#KonceptTVUpdates