Shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco siku ya jana tarehe 30 agosti limeuhabarisha umma kuwa kutakuwa na mgao wa umeme katika baadhi ya maeneo kutokana na maboresho ya mitambo ya msongo wa kilovoti 132 Mbagala-Dege ambapo maboresho hayo yatafanyika siku ya ijumaa na jumapili kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni.
Maeneo ambayo yataathirika ni Pamoja na Mbagala, Bandarini, Kurasini, Dege, Kibada, Mji Mwema, Kisarawe , Pemba Mnazi, Avic Town, Tuangoma na Geza Ulole.
#KonceptTVUpdates