Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia kijana mmoja, mkazi wa Mtaa wa Tambukareli, mjini Geita, kwa tuhuma za kumuua kijana mwenzake kwa kumchoma na kisu mara mbili kifuani wakati wakidaiana Sh5, 000.
RPC wa Geita, Safia Jongo amesema Abubakar alikuwa akidai deni la shilingi 5000 baada ya kazi ya kuchinja na kuchuna mifugo katika machinjio ya Serikali Kata ya Mtakuja na tukio Hilo lilitokea Agosti 27, 2023.
“Walikuwa wanadaiana deni la shilingi 5000 baada ya kazi ya kuchinja na kuchuna mifugo ambayo ilichinjwa yaani hawa ni Wachunaji wako pale machinjio kama Wachunaji kwahiyo baada ya malipo ndio wakaanza kugombania hiyo 5000”
“Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi huku upelelezi ukiendelea ambapo kwa taarifa za awali Mtuhumiwa huyo alimchoma Abubakari kifuani mara mbili kwa kutumia kisu ambacho alikuwa akikitumia kufanyia kazi hiyo katika machinjio”
#KonceptTVUpdates