Shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco limetoa taarifa kwa umma siku ya jana kuwa kutakuwa na mgawo wa umeme kwa baadhi ya mikoa hapa nchini, hii ni kutokana na maboresho yanayoendelea.
Shirika hilo la Umeme limesema njia ya umeme itakayozimwa ni kutoka Kidatu kwenda Kihansi kwa siku mbili kuanzia Agosti 26 hadi 28, 2023
Umeme utakuwa wa mgawo kwa Saa 12 kuanzia Saa 1 Asubuhi hadi 12 Jioni huku Mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Songwe, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga, Tabora, Simiyu, Mwanza, Geita na Mara ikitarajiwa kuathirika.
Sababu za kuzimwa kwa njia hiyo ni kuruhusu mkandarasi anayejenga kituo kipya cha kupooza umeme Ifakara kuunganisha kituo hicho kwenye gridi ya taifa. Kazi hiyo itaruhusu kuunga msongo wa njia ya kilovoti 220 Kihansi-Kidatu kwenye kituo kipya.
#KonceptTVUpdates