Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) imetangaza matokeo ya Urais siku ya jumamosi ambapo Emmerson Mnangagwa ameshinda na hivyo kutetea Kiti chake kwa 53% ya Kura zilizopigwa.
ZEC imesema Mpinzani Mkuu wa Mnangagwa, Nelson Chamisa anayeongoza chama cha Citizens’s Coalition for Change (CCC), alipata 44% ya kura za Urais, hata hivyo Chamisa amekataa Matokeo hayo.
Hatua hii inakuja ikiwa ni muda mfupi tangu Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU OEM) kutangaza kuwa Uchaguzi huo haukuwa Huru na Haki, huku baadhi ya Waangalizi wa Uchaguzi huo wakikamatwa. Mnangagwa aliingia Madarakana mara ya kwanza mwaka 2017 kwa kumpindua Robert Mugabe.
Alipoidhinishwa kuwa rais kwa mara ya kwanza, Mnangagwa ambaye pia anajulikana kama “Mamba” aliahidi mwanzo mpya kwa raia wa nchi yake.
Lakini Zimbabwe ni nchi mojawapo iliokabiliwa na mfumko wa bei wa kiwango cha juu duniani mwezi uliopita bei za bidhaa Julai zilipanda kwa 101.3% tangu mwaka uliopita. Bado kuna ukosefu wa ajira wakati ni 25% ya wananchi walio na kazi rasmi.
Ahadi ya Mnangagwa kuhakikisha haki za binaadamu pia inaonekana kutokuwa na mashiko, huku kukiwa na mageuzi kidogo tangu kuondoka kwa Mugabe. Wakosoaji wanasema kiongozi huyo wa miaka 80 amenyamazisha na kukandamiza upinzani kuelekea uchaguzi huo ambao alitarajiwa pakubwa kushinda.
Tume ya uchaguzi Zimbabwe (ZEC) inasema mpinzani mkuu wa Mnangagwa mgombea kutoka chama cha Citizens’ Coalition for Change (CCC) Nelson Chamisa, alijinyakulia 44% ya kura.
Mnangagwa alijipatia zaidi ya kura milioni 2.3, naye Chamisa akijipatia kura milioni 1.9, kwa mujibu wa ZEC. Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura katika nchi ilio na jumla ya raia milioni 16 ilikuwa ni 69%, tume hiyo imesema.
Upinzani unadai kulikuwa na udanganyifu, lakini mahakama ya katiba imeidhinisha matokeo hayo.
#KonceptTVUpdates