Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina amelishauri bunge kutopitisha Azimio la Bunge kuhusu itifaki ya biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wa Mwaka 2012 kwenye mkutano wa 12 wa bunge.
Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma hii leo Alhamisi, Agosti 31, 2023 alipokuwa akichangia maoni juu ya mjadala huo ambapo pia amelikumbusha bunge kuwa mjadala huo ulikuwapo tangu awamu ya nne iliyoongozwa na rais mstaafu dkt Jakaya Kikwete.
Aidha mpina amesema ripoti haioneshi wazi juu ya namna ambayo taifa linakwenda kunufaika na huduma sita ambazo zimeorodheshwa kwenye ibara ya 16 (b) ikiwemo biashara, tehama, ujenzi licha ya kwamba biashara hizo zinafanyika.
Lakini pia Mpina amezungumzia juu ya fursa ambazo ni za kawaida sana na zinaweza kufanywa na watu ambao wapo ndani ya jumiya ya SADC ambazo wamekuwa wakipatiwa watu kutoka Ulaya na Asia huku pia akigusia suala la kuadimika kwa dola nchini ambapo kwa maoni yake amesema tatizo hilo linatokana na ufisadi wa trilioni 280 ulioripotiwa na FIU.
#KonceptTVUpdates