MWANAMKE aliyeshiriki katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya kuchanganya udongo, Khadija Abbas Rashid amefariki dunia jana Jumanne Agosti 23, 2023 nyumbani kwake Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi akiwa na umri wa miaka 74.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano ambapo wametoa taarifa hiyo katika mitandao yao mbalimbali ya kijamii.
Kwa upande wake, binti wa marehemu Aziza Makarani akielezea msiba huo amesema mama yake amefariki leo Jumanne majira ya 8:30 mchana akiwa nyumbani kwao Rahaleo katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Marehemu alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika sherehe ya mfano ya kuchanganya udongo kutoka Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26 mwaka 1964.
Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Julius Nyerere na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Abeid Karume ziliungana na kuunda Tanzania.
#KonceptTVUpdates