Mwani ni aina ya mimea inayoota na kukua kwenye maji chumvi (bahari) na maji baridi (mito, maziwa na mabwawa). Tofauti iliyopo kati ya mwani na mimea mingine inayokua kwenye nchi kavu ni kwamba mwani hautegemei mizizi kufyonza maji na virutubisho vingine bali hutumia sehemu zote za mmea kuvyonza virutubisho vinavohitajika kutoka kwenye maji.
Aina ya jamii ya mwani inayolimwa nchini Tanzania kitaalam hujulikana kama “Eucheuma denticulatum” na pia huitwa Eucheuma spinosum. Aina nyingine ni “Kappaphycus alvarezii” kwa jina jingine Eucheuma cottonii.
Aina hizo za Mwani hustawi vizuri Sana katika ukanda huu, hususani ukanda wa kaskazini na kusini mashariki mwa bahari ya Hindi. Hii inatokana na hali nzuri ya mazingira ya bahari yanayosaidia ustawi wake na kufanya wakulima wa Mwani kupata Mwani wa kutosha katika kipindi cha mavuno.
Vikundi vingi vya wanawake hujishughulisha na kilimo cha zao hili huku wakisaidiwa na wataalamu wa Mwani ili kujikwamua kiuchumi pamoja na kupata chakula kwaajili ya familia zao.
Sambamba na hayo, Mwani hustawi vizuri pia kwenye maji baridi ikijumuisha maeneo ya mito, maziwa na mabwawa japokuwa makala hii itajikita zaidi kuzungumzia Mwani unaostawi katika maeneo ya bahari.
Ukiwa katika fukwe za bahari Mwani huwa na rangi mbalimbali zinazoipamba bahari na kuifanya iwe ya kuvutia na kubwa kuliko yote ni kwamba Mwani ni viumbe hai wa bahari ambao hawatumii tu mizizi katika kufyonza virutubisho ila hutumia sehemu zote katika kufyonza virutubisho na kufanya ustawi wake kuwa mzuri bila kutegemea mizizi kwa kiasi kikubwa kama ilivyo mimea mingine ya baharini na nchi kavu.
Mwani huwa na rangi ya kijani, kahawia na nyekundu. Rangi hizo zimekuwa zinasababishwa na kuongezeka au kupungua kwa kina cha maji ya bahari.
FAIDA ZA MWANI KIAFYA
- Inatengeneza kinga ya mwili
Hali mbaya ya maji ya pwani ambamo mwani huweza kustawi ili kuendelea kuishi imemaanisha kuwa mwani kuwa na virutubisho ambavyo pia huweza kumlinda mlaji na magonjwa mbalimbali kwa kuhakikisha kinga yake inakua na nguvu. Pia husaidia urekebishaji wa kinga na uboreshaji wa mwitikio wa kinga kwa walaji.
- Huboresha udhibiti wa sukari kwenye damu
Uchunguzi unaonyesha kuwa mwani husaidia udhibiti wa sukari ya damu na uwezekano wa kupunguza hatari ya kisukari cha aina ya 2. Hii ni shukrani, kwa kiasi, kwa misombo kama vile carotenoid na fucoxanthin, ambayo husaidia kupunguza upinzani wa insulini na kusaidia udhibiti bora wa sukari kwenye damu.
Maudhui ya nyuzinyuzi nyingi katika mwani pia hucheza sehemu yake katika kusaidia kupunguza kasi ya usagaji chakula.
- Husaidia afya ya moyo
Mwani, ni muhimu kwa afya, na hasa kwa moyo na mfumo wa moyo. Uchunguzi unaonyesha kwamba mwani unaweza kuboresha usawa wa cholesterol na kufanya kazi kama damu nyembamba, kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.
- Husaidia afya ya tezi
Tezi ina jukumu la kutoa homoni ili kusaidia kutawala ukuaji wetu, nishati, uzazi na ukarabati.
Ili kufanya hivyo, tezi huhitaji idadi ya virutubisho, moja ambayo ni iodini na nyingine asidi ya amino, tyrosine. Virutubisho hivi vyote viwili hupatikana katika mwani, ingawa katika viwango tofauti kulingana na aina na jinsi unavyohifadhiwa na kutayarishwa.
#Makala, KonceptTVUpdates