Benki ya NBC yakabidhi Basi Jipya Lenye Thamani ya Sh ya Mil 470 kwa Klabu ya Singida Fountain Gate FC. Benki hiyo imekabidhi basi jipya kwa timu ya Singida Fountain Gate FC ya mkoani Singida inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC ikiwa ni mwendelezo wa dhamira ya dhati ya Benki ya NBC katika kuboresha Ligi Kuu ya NBC.
Singida Fountain Gate FC inakuwa klabu ya pili inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC kunufaika na mpango huu unaohusisha mkopo nafuu kutoka kwa mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC baada ya klabu ya KMC ya Kinondoni kunufaika na mpango kama huu mwezi Februari mwaka huu.