Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri na Makatibu Wakuu, hatua ambayo imekuwa na athari kubwa katika muundo wa serikali. Katika mabadiliko haya, Mhe. Rais ameanzisha nafasi mpya ya Naibu Waziri Mkuu na kuifuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na badala yake kuunda Wizara mpya mbili za Ujenzi na Uchukuzi.
Aidha, ameimarisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuongeza nafasi za Naibu Waziri na Katibu Mkuu watakaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
Katika mabadiliko haya, Mhe. Rais ameteua viongozi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, na Naibu Makatibu Wakuu.
#KonceptTvUpdtes