Kupitia mitandao ya kijamii Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza Askofu Dkt. Alex Malasusa kwa kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mara baada ya uamuzi wa wajumbe 214 kati ya 248 wa mkutano mkuu wa 21kumchagua na kisha kuchukua nafasi ya Askofu Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozi kwa mujibu wa katiba ya kanisa hilo.
Nakupongeza Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa kwa kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Kuchaguliwa kwako ni ishara ya imani ya Kanisa juu yako katika kulitumikia.
Kwa hakika, wito wako huu si tu utumishi katika yahusuyo roho na imani, lakini pia katika yote yanayofanywa na Kanisa kuboresha maisha ya Watanzania sehemu mbalimbali.
Nanukuu kutoka Biblia Takatifu kwenye Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 31:8 inayosema: “Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.”
Nakutakia kila la kheri.
#KonceptTVUpdates