Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kuendana na mabadiliko ya dunia.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakatia kifunga mafunzo ya viongozi hao kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere.
Aidha, Rais Samia amewataka viongozi hao kuwa wepesi kukabiliana na mabadiliko hayo ili kuendana na mfumowa kidunia wa kisiasa na kiuchumi bila kusubiri maelekezo kutoka juu.
Vile vile, Rais Samia amewataka viongozi huo kujiamini na kuwa na hoja ya kutetea maamuzi wanayoyafanya kwa maslahi ya wananchina taifa kwa ujumla kwa kuzingatia miongozo, kanuni na sheria.
Rais Samia pia amewataka kuhakikisha usalama wa vijana kwa kusimamia miradi inayowahusisha ambayo mingi hutumika kupenyeza ajenda zinazopotosha maadili ya vijana na utamaduni wa taifa.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kuacha kupuuza wananchi hivyo wawatumikie kwa kuwa hudumia na kushughulikia kero, malalamiko na mahitaji yao.
Hali kadhalika, Rais Samia amewataka watumishi serikalini katika idara tofauti kwenye ngazi za mikoa kutumia fedha za maendeleo zinazotolewa kwa maslahi ya wananchi.
#KonceptTVUpdates