Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan siku ya jana amezindua rasmi tawi la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Waziri mkuu, spika wa bunge, mawaziri na wananchi kwa ujumla Pamoja na watu kutoka mataifa tofauti tofauti ambapo siku ya jana ilikuwa ni kilele cha shamrashamra za kizimkazi.
Akitoa maelezo ya awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna, amemueleza Mhe. Rais kuwa kupitia tawi hilo, wakazi wa Paje na maeneo jirani watapata huduma zote za kifedha ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu na pia Azma yetu ni kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma bora za kifedha!
#KonceptTVUpdates