Baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya JKU, Singida Big Stars jana ilikuwa na kibarua kigumu cha kusaka tiketi ya kutinga raundi ya kwanza wakati iliporudiana na wawakilishi hao wa Zanzibar katika Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1:30 usiku.
Timu ya Singida Big Stars ilipata kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar katika mchezo wa marudiano Kombe la shirikisho barani Afrika, ukipigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Matokeo haya yanaifanya Singida ifuzu hatua inayofuata kwa jumla ya magoli 4-3 kufuatia ushindi wa 4-1 iliyoupata katika mchezo wa kwanza. Magoli ya JKU yametoka kwa Nassor Juma dakika ya 7 na Gamba Matiko dakika ya 42 kwenye dakika arobaini na tano za kipindi cha kwanza.
Kocha wa Singda BS, Hans Pluijm alizungumza kabla ya mechikuwa licha ya ushindi mnono walioupata katika mechi ya kwanza,amewatengeneza kisaikolojia wachezaji wake ili wasibweteke leo.
“Tunatakiwa tusiamini kwamba tumeshafika sehemu ambayo tunaitaka. Yale matokeo ya kwanza tumeshasahau na sasa tunataka ushindi kwenye mchezo huu,”alisema Pluijm.