Mganga Mkuu wa hospitali ya CCBRT Dkt. Cyprian Ntomoka ametoa tahadhari kwa wale wanaotumia kope bandia ili kuepukana na magonjwa ya macho.
Ambapo ameshauri kuwa kwa wale wote wenye uhitaji wa kuweka kope bandia wanapaswa kuwaona wataalamu wa tiba ili kupatiwa vipimo vya macho ili kuepuka ugonjwa wa macho kwani watu wengi huenda kutibiwa macho kutokana na utumiaji huo wa kope bandia.
Dk Cyprian amesema hayo leo Agosti 30, 2023 Jijini Dar es Salaam alipofanya mahojiano na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali ambao pia walitembelea hospitali na kujionea kazi na huduma zitolewazo kwa watanzania hospitalini hapo.
Aidha wahariri hao wamesema kuwa ukweli ziara hiyo hospitalini hapo imewafungua macho, ambapo awali walidhani kuwa CCBRT ni hospitali ya macho na kutibu ulemavu mbalimbali na hatimaye kutambua kuwa inatoa huduma nyingi za kibingwa na bobezi zikiwemo huduma za afya ya uzazi.
#KonceptTVUpdates