ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 30, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

TANZANIA NA INDONESIA ZATIA SAINI HATI SABA

By Shukran Suzo - Aug 23, 2023 In habari

SUZO SHUKRANI by SUZO SHUKRANI
Aug 23, 2023
in HABARI
0
TANZANIA NA INDONESIA ZATIA SAINI HATI SABA
0
SHARES
27
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Kufuatia taarifa iliyotolewa jana na idara ya kurugenzi ya mawasiliano ikulu imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia uamuzi wa Serikali ya Indonesia wa kufufua shughuli za Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima Vijijini (FARTC) kilichopo Mkindo mkoani Morogoro.

RelatedPosts

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

Sep 29, 2023

TSO WAZINDUA GALA DINNER

Sep 29, 2023

CHANJO YA MBWA NI MUHIMU

Sep 29, 2023
Load More

Rais Samia amesema hayo jana akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Joko Widodo aliyepo nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili wakati wakizungumza na vyombo vya habari. Aidha, Rais Samia amesema kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 1996 na Serikali ya Indonesia kimechangia kwa kiasi kikubwa kuelimisha wakulima na kutoa mafunzo kwa wataalam wa kilimo.

Rais Samia pia amesema Tanzania na Indonesia zimekubaliana kukuza biashara na uwekezaji kwa kuzileta pamoja sekta za umma na binafsi ili kuimarisha ushirikiano katika viwanda, kilimo, nishati, madini, mafuta na gesi, uvuvi na utalii.

Vile vile, Rais Samia amesema majadiliano yao yamebainisha nia ya Tanzania kupata uzoefu wa uzalishaji mafuta kutoka kwa Indonesia ambaye ni mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta ya mawese duniani.

Hali kadhalika, Rais Samia amesema Serikali ya Tanzania imejidhatiti kuhakikisha inaongeza uzalishaji wa mafuta ya kula ili iache kabisa kutumia fedha zake za kigeni kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi.

Nchi hizo mbili zimetiliana saini hati 7 za Makubaliano (MoUs) ikiwemo sekta za ulinzi, nishati, kilimo, mifugo, uvuvi na uchumi wa buluu, madini, na pia misamaha ya viza kwa wamiliki wa hati za kusafiria za kidiplomasia na za huduma.

Hati za Makubaliano kati ya Tanzania na Indonesia kwa upande wa nishati zilitiwa saini na Waziri wa Nishati January Makamba na Waziri wa Nishati na Madini wa Indonesia Arifin Tasrif Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 22 Agosti, 2023.

 

#KonceptTVUpdates

Related

SUZO SHUKRANI

SUZO SHUKRANI

Related Posts

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO
HABARI

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TSO WAZINDUA GALA DINNER
HABARI

TSO WAZINDUA GALA DINNER

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
CHANJO YA MBWA NI MUHIMU
AFYA

CHANJO YA MBWA NI MUHIMU

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN
HABARI

52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA
HABARI

SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 
HABARI

TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 

by I am Krantz
Sep 29, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

August 2023
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In