Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya hali ya hewa kali kwa siku tatu, ikitabiri kutokea kwa upepo mkali na mawimbi makubwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa, kuna uwezekano wa upepo mkali kufikia kasi ya kilomita 40 kwa saa au zaidi na mawimbi kufikia urefu wa hadi mita 2.
Hali hii ya hewa inatarajiwa kuathiri maeneo ya mwambao wa Bahari ya Hindi, ikiwemo mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mikoa mingine inayoweza kuathiriwa na hali hii ya hewa ni maeneo yanayozunguka Ziwa Victoria, ikiwemo mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, na Mara, pamoja na mikoa inayozunguka Ziwa Tanganyika, kama Kigoma, Katavi na Rukwa.
Kutokana na hali hiyo, TMA inatoa wito wa kuchukua tahadhari, hasa kwa wale wanaofanya shughuli za baharini na ziwani, wakiwemo wasafiri wanaotumia njia hizo.
#konceptTvUpdates
#TMA