Jeshi la Polisi Tanzania linatafuta James Fabian Urasa kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanafunzi katika Shule ya Msingi Samanga, Wilayani Rombo. Inadaiwa alimpa adhabu ya viboko ambayo ilisababisha kifo cha mwanafunzi huyo. Mtuhumiwa ametoroka na juhudi za kumkamata zinaendelea.
Inadaiwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 17, 2023 na kutokomea kusikojulikana
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema “Mtuhumiwa alimpa adhabu ya viboko Mwanafunzi baada ya kupiga kelele, aliporejea kwenye dawati lake Mwanafunzi akaanza kujisikia vibaya na ndipo wakampeleka hospitali, akiwa huko akafariki Duniani.
“Baada ya Mwalimu kusikia hivyo, akazima simu na kukimbia, tumemtafuta hatujafanikiwa, juhudi zinaendelea kumtafuta ndio maana tumetoa tangazo hilo, ni bora angebaki kwa kuwa inawezekana Mtoto alikuwa na changamoto zake nyingine za kiafya lakini kitendo cha yeye kukimbia inamaanisha kuna kitu kibaya alichomaanisha.
#KonceptTvUpdates
#Polisi_tanzania