Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Mohamed Janabi amewataka wafamasia kuzingatia uaminifu pamoja na weledi katika utendaji kazi wao wa kila siku.
“Maisha ni mbio ndefu (marathon) na mafanikio ni matokeo ya mchakato wa kitambo fulani, usijaribu kudhani maisha ni mbio ya mita mia kwa kujiingiza kwenye vitendo vya wizi wa dawa, hospitali haitavumilia mtumishi wa aina hii akikamatwa atawajibishwa ipasavyo” amesema Prof. Janabi
Prof. Janabi ameyasema hayo jana wakati wa hafla la kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya nne iliyoandaliwa na Idara ya Famasi MNH ambapo Wafamasia watatu Faraji Chambuso, Seleman Madebe na Scholastica Chimani walitunukiwa vyeti na zawadi.
Aidha amepongeza idara nzima ya famasi kwa kufanya kazi kwa bidii jambo ambalo limepelekea kupunguza changamoto ya upungufu wa dawa na kupunguza foleni kwenye madirisha ya dawa.
#KonceptTVUpdates