Kufuatia masaa takribani 12 tangu Watu nane wakiwemo Watoto sita na Walimu wawili ambao walikuwa wamekwama baada ya kivuko cha angani kupata kaskazini-magharibi mwa nchini Pakistan wameokolewa.
Jitihada za uokoaji zilianza baada ya Watoto hao sita na Walimu wawili waliokuwa wakisafiri kwenda Shule kunasa kwenye usafiri huo ambao hutegemea nyaya na kebo kuwasafirisha ambapo kwa bahati mbaya baadhi ya nyaya hizo zilikatika na kuwaacha hewani bila msaada wowote.
Uokoaji huo ulijumuisha helikopta za kijeshi na utumiaji wa kamba lakini usiku ulipoingia Mamlaka za Pakistani zililazimika kusitisha uokoaji wa helikopta huku pia upepo mkali ukichangia kuchelewesha uokoaji.
Watoto wengi wanaoishi maeneo ya mbali na milimani katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa hutegemea magari ya kebo kuwasafirisha kwenda shuleni na kurudi.
Hata hivyo Polisi nchini humo wamemkamata mmiliki wa gari hilo la kebo Gul Zareen kwa mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha na uzembe.
Kukamatwa huko kumekuja baada ya mmoja wa watoto aliyekuwa amenasa kuzungumza na kusema kuwa alihofia kuwa ulikuwa “ndio mwisho wake” wakati wa mkasa huo.
#KonceptTVUpdates