Takriban watoto 498 nchini Sudan na huenda mamia zaidi wamekufa kutokana na njaa, wakiwemo watoto dazeni wawili katika kituo cha watoto yatima cha serikali, huku huduma muhimu zikikosa chakula au kufungwa, lilisema shirika la Save the Children.
Tangu vurugu zilipoanza mwezi Aprili, Shirika la Save the Children limelazimika kufunga vituo vyake 57 vya lishe, huku watoto 31,000 wakikosa matibabu ya utapiamlo na magonjwa yanayohusiana na hayo kote nchini. Katika vituo 108 shirika bado linafanya kazi, hifadhi ya chakula cha matibabu inapungua sana, na hifadhi ya akiba, au vifaa vya dharura, sasa vinatumika katika hali mbaya zaidi.
Katika jimbo la Gedaref mashariki mwa Sudan, kwa uchache watoto 132 walikufa kutokana na utapiamlo kati ya Aprili na Julai, huku asilimia 36 ya visa vyote vya watoto waliolazwa katika hospitali moja ya serikali wakiwa na hali ya kufa kutokana nayo au magonjwa yanayohusiana nayo.
Hospitali hiyo pia imeripoti ongezeko kubwa la visa vya utapiamlo, huku watoto waliokimbia makazi yao hivi majuzi kutoka Khartoum na wanaoishi katika kambi duni wakiathirika haswa.
Katika jimbo la White Nile, takribani watoto 316 wengi wao wakiwa chini ya miaka mitano, walikufa kutokana na utapiamlo au magonjwa yanayohusiana kati ya Mei na Julai, na zaidi ya kesi 2,400 za watoto wenye utapiamlo mkali aina mbaya zaidi ya utapiamlo walilazwa kwenye vituo vya lishe tangu mwanzo wa mwaka.
Huko Khartoum, takriban watoto 50, wakiwemo watoto walikufa kwa njaa au magonjwa yanayohusiana nayo katika kituo cha watoto yatima cha serikali baada ya mapigano kuwazuia wafanyakazi kuingia kwenye jengo hilo ili kuwatunza.
Maghala mengi ya kuhifadhi chakula kwa ajili ya WFP pamoja na mashirika ya misaada kama vile Save the Children yamevamiwa tangu kuanza kwa mzozo huo, na WFP ilitangaza mwezi Mei kwamba angalau dola za Marekani milioni 14 za chakula zimeporwa. Malori mengi ya WFP pia yanacheleweshwa katika maeneo ya mpakani, na hivyo kuzidisha hali ya mzozo.
#KonceptTVUpdates