Mradi wa maji wa Mji wa Kaliua ambao thamani yake ikiwa ni zaidi ya shilingi milioni 503, ujenzi wake umefika asilimia 93 na kuanza kutoa huduma ya majisafi kwa wananchi.
Mradi huo pamoja na kazi nyingine, umehusisha ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 50,000 ujenzi wa raiser yenye urefu wa mita 12 na ulazaji wa bomba zenye urefu wa km 13.5 Mradi huu ni suluhisho la huduma ya majisafi kwa wananchi wakati mradi mkubwa utakaotumia maji ya ziwa Victoria ukiendelea kutekelezwa.
Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua wamepongeza kazi inayofanywa na Serikali katika juhudi za Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa majibu ya changamoto ya huduma ya maji kwa wakati. Mkandarasi wa mradi wa miji 28 ameshakabishiwa na Serikali eneo la ujenzi wa mradi wilayani Kaliua.
#KonceptTvUpdates