Mbunge wa Tanga Mjini ambaye pia ni Waziri wa afya Ummy Mwalimu jana amekabidhi boti mbili kwa vikundi vya uvuvi ambavyo ni mwani na majongoo bahari vya mtaa wa Mchukuuni kata ya Tangasisi.
Boti hizo zenye thamani ya shilingi milioni 24. 5 kila moja sawa na milion 49 kwa boti zote mbili zimetolewa na Taasisi ya Botnar Foundation kufuatia ombi la Ummy alilotoa kwa Botna Foundation mnamo tarehe 17 /07/2023 wakati walipotembelea na kusikiliza maendeleo na kero za vikundi hivyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Ummy amewashukuru wadau hao na kuwataka wanavikundi hao wa Mchukuuni kutumia boti hizo katika kuinua kipato chao.
Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Mkurugenzi wa Botnar Foundation Dr Hassan Mshinda, Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga Ndugu Seleman Sankwa, Katibu Itikadi na Uenezi Wilaya ya Tanga na diwani wa kata ya Tangasisi Ahmed Mwijanga.
#KonceptTVUpdates