Wakati masabiki mbalimbali wa Yanga kote duniani wakiupokea msimu mpya wa ligi kuu ya NBC TANZANIA BARA, msisimko ni mkubwa sana. Yanga siku ya leo imeibuka na ushindi wa magoli 5 kwa 0 dhid ya timu ya “Watoza Ushuhuru”, KMC FC.
Mchezo uliopigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi, safari ya ushindi katika mehi hiyo ilianzishwa kwa kasi zaidi na Dickson Job aliyefunga goli la kwanza katika dakika ya 17, vijana wa Yanga wakisimamiwa na Miguel Gamond waliwachanganya zaidi “Watoza Ushuhuru'” hao kwa kuwakandamizia kipigo cha magoli 5 kwa hakuna (0), magoli ambayo yalionezewa na Ki Azizi 59′, Konkoni 71′, Mudathir 77′ na Pacome 80′.
Licha ya kukosekana kwa umakini mkubwa ka mshambuliaji Kenedy Musonda, ambaye adi anafanyiwa mabadiliko hakuweza kufunga katika mchezo jhuo, lakini Yang imeendelea kusimama imarana kufunga kiasi hicho cha magoli.
#KonceptTvUpdates