Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wamekutana na JKT ambao nao waliibuka mabingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita timu zote zikicheza mchezo wa pili wa ligi msimu huu.
Ubingwa huo wa Yanga msimu uliopita waliuchukua baada ya michezo 30 wakishinda mechi 25 sare 3 wakipoteza 2 wakikusanya jumla ya alama 78, wanakutana na JKT ambayo kwenye mechi zake 28 za msimu uliopita walishinda 20 wakitoa sare 3 na kupoteza 5 wakijikusanyia alama 63 kwenye ubingwa wao.
JKT iliianza ligi kwa kuichapa Namungo ugenini kwa bao 1-0 huku Yanga nao wakianza kwa kishindo kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KMC ukiwa ndio ushindi mkubwa mpaka sasa tangu ligi ianze msimu huu.
Mchezo uliochezwa jana kwenye dimba la azam complex chamazi majira ya saa moja usiku ulimalizika kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5 kwa 0.
Magoli hayo yakiwekwa kambani na Aziz Ki, Musonda, Yao, Pamoja na Max Nzengeli.
#KonceptTVUpdates