Upigaji kura unaendelea katika uchaguzi mkuu wa pili nchini Zimbabwe tangu mapinduzi ya mwaka 2017 yaliyomwondoa madarakani mtawala marehemu Robert Mugabe.
Wananchi wa Zimbabwe watachagua rais mpya, wabunge 210 wa kitaifa na viongozi 1,970 wa serikali za mitaa na manispaa.
Zimbabwe inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi na raia wengi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika wanaweka matumaini yao ya mustakabali mzuri kwenye uchaguzi wa rais Ulionza mapema hii leo Agosti 23, 2023.
Watu milioni 6.6 waliosajiliwa kuwa wapiga kura wanatarajiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ambao umetabiriwa kuwa utasababisha mgawanyiko.
Katika miaka ya hivi karibuni, maeneo ya mijini yamekuwa ngome za upinzani ikiwemo Mbare ambao ni mtaa mkongwe wa mji mkubwa unaotarajiwa kushuhudia ushindani mkubwa.
Katika eneo la Mbare, bango kubwa lenye picha ya Mnangagwa linaning’inia kwenye ukuta wa nyumba moja iliyoko kwenye mojawapo ya vitongoji duni vya Harare. Ujumbe kwenye bango hilo unawarai watu kumchagua Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80 kuwa rais kwa muhula wa pili.
Bango hilo liko mkabala ya barabara ambayo haijawekwa lami, na ambayo sehemu yake imetapakaa maji taka. Kando yake ni wafanyabiashara wa mkaa.
#KonceptTVUpdates