Kupitia taarifa iliyosomwa kwenye TV ya serikali jana Jumatano ya septemba 6,2023 jioni Viongozi wa kijeshi wa Gabon wametangaza kusitisha kifungo cha nyumbani cha Rais Ali Bongo aliyeondolewa madarakani, wakisema kuwa sasa “yuko huru kutembea apendavyo.”
Msemaji wa Jeshi Kanali Ulrich Manfoumbi alisema uamuzi wa kumwachia huru Ali Bongo ulitokana na “hali yake ya afya na kuongeza kuwa anaweza, ikiwa anataka, kusafiri nje ya nchi kwa uchunguzi wa matibabu.”
Tangu jeshi lilipofanya mapinduzi Agosti 30, lilimweka Rais huyo wa zamani katika kizuizi cha nyumbani, na kutangaza kuwa wanadhibiti nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.
Uamuzi wa kumwachilia huru unafuatia shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kikanda ya Afrika ya Kati ECOWAS na majirani wa Gabon, kuheshimu uadilifu wa kimwili wa kiongozi huyo wa nchi aliyeondolewa madarakani.
Mnamo 2018, Ali Bongo alipatwa na kiharusi. Afya yake ilikuwa chanzo cha wasiwasi kwa wengi katika maandalizi ya uchaguzi wa Rais wa 2023.
#KonceptTVUpdates