Mahakama ya Mkoa wa Vuga, jana tarehe 04/09/2023 imemhukumu mshtakiwa Haji Saleh Omar, mme, (20) Mshirazi na mkazi wa Makadara Zanzibar kutumikia kifungo cha miaka 15 Chuo cha Mafunzo na kulipa fidia ya shilingi Milioni Moja kwa kosa la Kulawiti.
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani tarehe disemba 22, 2021 na kupewa kesi namba 344/2021 ambapo awali mshtakiwa huyo alishtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 5 kinyume na kifungu namba 115(a) cha sheria ya adhabu 6/2018 Sheria ya Zanzibar.
Mnamo disemba 04, 2021 majira ya saa 2:00 asubuhi huko Makadara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, mshtakiwa alimuingilia mtoto wa kiume jambo ambalo ni kosa kisheria.
Akisoma maelezo ya hukumu, hakimu wa mahakama hiyo Nayla Abdulbasit Omeyar amesema Mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita ambao haukuwa na chembe ya shaka ambao umemtia mshtakiwa hatiani.
#KonceptTVUpdates