Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu kifungo cha Miaka 20 aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt John Pima na wenzake wawili baada ya kukutwa na hatia kwenye makosa ya uhujumu uchumi.
Hukumu hiyo imetolewa jana Agosti 31, 2023 Hakimu Seraphin Nsana wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha baada ya kujiridhisha pasina Shaka juu ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kwa pande zote mbili.
Wengine Waliohukumiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.
Hakimu Nsana amesema hukumu hiyo ameitoa kwa kuzingatia sheria, baada ya Maombi ya Mawakili ya Pande zote mbili, ikiwemo washtakiwa kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, kutegemewa na Familia, pamoja na ushirikiano walioutoa kwa kipindi chote cha mwenendo wa Kesi.
Hata hivyo dkt John Pima na Wenzake wana haki ya kukata rufaa endapo hawajaridhishwa na hukumu hiyo.
Dkt Pima na Wnzake walikuwa Wakikabiliwa na mashataka 9 ikiweno ya utakatishaji wa kiasi cha milioni 103.
#KonceptTVUpdates