Benki ya NMB imetoa vifaa vya michezo jana tarehe 1 septemba 2023 kwa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo kwa kutambua umuhimu wa mazoezi kwa afya ya jamii, benki imetangaza udhamini na kukabidhi vifaa vya michezo kwa Waheshimiwa Wabunge vyenye jumla ya thamani ya Sh. Milioni 130 kwa ajili ya Bonanza la Wabunge litakalofanyika leo (Septemba 2), ndani ya Viwanja vya John Merlin, Jijini Dodoma.
Vifaa hivi vimepokelewa na Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Mhe. Festo Sanga, aliekabidhiwa na Meneja waw a benki hiyo Kanda ya Kati Janeth Shango na kushuhudiwa na waheshimiwa wabunge na wafanyakazi wa NMB.
Aidha NMB imewatakia Waheshimiwa Wabunge na watumishi wa Bunge, Bonanza jema lenye kuimarisha afya ili kuendelea kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi.
#KonceptTVUpdates