Baraza la Sanaa nchini Tanzania BASATA limetoa taarifa juu ya Sakata ambalo limeshika vichwa mbalimbali vya Habari nchini juu ya tuhuma zilizotolewa na msanii wa bongo fleva Nay wa mitego kufungiwa kufanya tamasha bila ya kupewa taarifa kutoka sehemu husika.
Basata kupitia mwanasheria wake Christopher Kamgisha amesema kuwa sababu ya kuzuia tamasha hilo ni kutokana na msanii huyo kutotii wito mara mbili ambao ulimtaka afike ofisi hizo za basata tangu kipindi cha mwezi wa saba mara baada ya kutoa wimbo wa Amkeni.
Maelezo hayo yametolewa jijini dar es salaam kwenye ofisi za basata zilizopo ilala mbele ya waandishi wa Habari septemba 6,2023 ambapo mwanasheria ameongeza kuwa basata haihusiki na chochote juu ya msanii huyo kuitwa na jeshi la polisi nchini Tanzania kwani wao kama basata wanahusika na maadili ya Sanaa peke yake.
#KonceptTVUpdates