Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa baadhi ya mazao ikiwemo mchele, maharage na mahindi ambayo Tanzania ikiamua kutoyauza nje ya Nchi, mataifa mengi yatapiga kelele kutokana na kuwa Tanzania ina mchango mkubwa kwenye uzalishaji wa mazao hayo kwa wingi.
Bashe amesema hayo jana Ikulu Dar es salaam wakati akiongea na Viongozi pamoja na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023), unaotarajiwa kufanyika Sept 05-08,2023 Jijini Dar es salaam.
“Tukizuia kuuza nje mchele Nchi nyingi za Afrika ambazo zinanunua mchele Tanzania zitapiga kelele, tukisema tunazuia kuuza nje maharage kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi nyingi zilizopo ukanda wa SADC ukiitoa Afrika Kusini Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje watapata shida sana”
“Kwahiyo yapo mazao ambayo tukisema hatuuzi itakuwa ni ishu, yapo mazao kama Nchi tunafanya vizuri na ndio malengo ya Serikali, sisi sasa hivi kama Serikali na ni maelekezo ya Mh. Rais tunaondoa ile dhana inayoitwa mazao ya chakula na biashara, mazao yote ya kilimo ni ya biashara, Mkulima anapoenda kulima mpunga sio tu kwa ajili ya kula na Familia yake ni biashara yake pia”
#KonceptTVUpdates