Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema Tanzania imepata mkopo wa Dola za Marekani milioni 300 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 700 kutoka Benki ya Dunia (World Bank – WB), fedha zitakazotumika kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo nchini.
Ameyasema hayo jana septemba 6,2023 jijini dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Programu ya Uvumilivu wa Mifumo ya Chakula Tanzania ambapo Programu hiyo imepangwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitano, hivyo ataweka jitihada zaidi ikamilike ndani ya miaka mitatu.
Ameongeza kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwenye maeneo walipo Wakulima wadogo.
Aidha, Waziri Bashe amesema moja ya matokeo ya programu hiyo ni kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa zaidi ya hekta elfu 37 na hivi sasa wizara hiyo imekwishaanza upembuzi yakinifu kwa ajili ya programu hiyo.
#KonceptTVUpdates