Benki ya NBC imezindua logo mpya ya Ligi Daraja la Kwanza ya Tanzania, inayojulikana kama “NBC Championship.” Uzinduzi huo ulifanyika leo katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa soka, wachezaji, na wadau wa mchezo huo.
Logo mpya ya NBC Championship inaonesha umoja, ufanisi, na ukuaji wa soka la daraja la kwanza nchini Tanzania. Benki ya NBC imejitolea kuendeleza na kukuza mchezo wa soka kwa kuwa mlezi wa ligi hii, na uzinduzi wa logo mpya ni hatua muhimu katika kufikia lengo hilo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi kutoka benki ya NBC, Elibariki Masuke “Tumeamua kuipa jina la NBC Championship League”. Aliongeza kuwa, “mnamo tarehe moja agosti mwaka huu, kwa mara nyingine tena Tanzania ilishuhudia utiaji saini wa TZS bilioni 32.6 ikiwa ni makubaliano mapya ya miaka mingine itano ya udhamini wa ligi kuu Tanzania bara”.
NBC Championship ina jukumu muhimu katika kukuza soka la Tanzania na kuibua vipaji vipya. Logo mpya inatarajiwa kutoa hamasa kwa wachezaji, mashabiki, na wadau wa soka kote nchini.
#KonceptTvUpdates