Benki ya NMB leo septemba 25,2023 imezindua hati fungani ya muda wa kati (Multicurrency medium term note – MTN) ya miaka 10 yenye thamani ya shilingi za kitanzania Trilion 1 ambayo itakuwa hati fungani ya pili kwa ukubwa barani Africa pia benki ya NMB imezindua hati fungani ya awamu ya kwanza “Jamii Bond” itakayodumu kwa miaka 3 kuanzia 2023-2026 ikitarajia kukusanya kiasi cha fedha za kitanzania 75 bilioni ambayo inakaribisha wawekezaji wote kununua bond kuanzia kiwango cha chini Tsh 500,000 na muwekezaji kupata riba 9.5%
Dirisha la uwekezaji wa Jamii bond limefunguliwa leo 25 September 2023 na litafungwa 27 Oktoba 2023 ambapo wawekezaji watanunua hati fungani hizo kupitia matawi yote ya NMB na kwa mawakala na madalali wa soko la mitaji kote nchini baada ya hapo itauzwa katika soko la hisa na mitaji la Dar es salaam (DSE)
Afisa mkuu wa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana CPA Nicodemus Mkama katika hotuba yake amesema CMSA imekubali kutoa kibali wa hati fungani ya muda wa kati Benki ya NMB yenye thamani ya billion moja baada mamlaka hiyo ilijiridhisha na kupitia taratibu zote za na kuona ni hati fungani yenye manufaa kwa wananchi.
Pia aliipongeza NMB kupitia hati fungani iliyopita ambayo iligawanya kwa matoleo manne huku hati fungani ya Jasiri ilikusudiwa kukusanya billion tisini na tano lakini ilikusanya billion mia mbili ishirini na kueleza kuwa benki hii imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi, kutoa gawio kwa wanahisa wake pamoja na kulipa kodi.
Hati fungani hii ya muda wa kati wa NMB yenye thamani ya trilioni moja imegawanyika katika maeneo matano Plan Vanila Bond,Miradi ya kijani, Uchumi wa buluu, Miradi ya kijamii na maendeleo endelevu.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NMB Bi Ruth Zaipuna amesema benki ya NMB itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wateja wetu hususani katika maendeleo endelevu. Akizungumzia kuhusu hati fungani ya Jamii amesema fedha hizi za uwekezaji zitakwenda kwenye miradi ya udhibiti wa uchafuzi mazingira, upatikanaji wa nishati mbadala, maji safi na salama, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula, Afya, elimu na uwezeshaji vijana, kusaidai miradi ya kijamii.
Msajili wa hazina Nehemia Mchechu amepongeza jitihada za uwekezaji chanya wa benki ya NMB ambayo yamechangia benki hii kukua na kuwa ya 3 katika ukanda wa Afrika mashariki huku ikitoa uwekezaji kwa wananchi moja kwa moja na serikali inaenda kujipanga kupitia mashirika mengine ya umma yaweze kukuza mitaji na kujiendesha.
#KonceptTVUpdates