Zaidi ya waendesha bodaboda 250 mkoani Dar es Salaam wamenufaika na mafunzo ya usalama barabarani yalioandaliwa na kutolewa na Kampuni ya betPawa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kitengo cha usalama barabarani.
Mafunzo hayo yamefanyika ijumaa tarehe mosi septemba 2023 yenye ujumbe ‘BetPawa na elimu ya Usalama Barabarani’ yanalenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupiga vita ajali za barabarani zinazoweza kuepukika na ambazo husababisha majeraha na vifo haswa kwa waendesha bodaboda ambao wamekuwa ni moja kati ya kundi linaloathirika sana.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja masoko wa betPawa Tanzania Bi. Borah Ndanyungu alisema takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa bodaboda ni kundi ambalo limekuwa likichangia sana katika ajali za barabarani huku akitaja uelewa mdogo wa sheria za usalama barabarani kuwa moja ya chanzo kikuu cha ajali hizo.
“Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 16,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani huku ajali za bodaboda zikichukua nafasi kubwa. Kutokana na ukweli huu, tumeona kuna haja ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kundi hili ambalo limekuwa ni muhanga wa ajali za barabarani,” amesema Ndanyungu.
Kwa upande wake SP Deus Sokoni ambaye ni Mkuu wa Dawati la Elimu, Kitengo cha Usalama Barabarani kutoka Jeshi la Polisi, aliipongeza kampuni ya kubashiri michezo ya BetPawa kwa kudhamini mafunzo hayo muhimu
“Sisi sote kwa pamoja ikiwa ni Pamoja na jeshi la Polisi, madereva, jamii nzima na wadau wote tuna wajibu wa kufanya barabara zetu ziwe salama. Ninayofuraha kuona BetPawa wamekuwa mstari wa mbele na kuamua kufadhili mafunzo haya ambayo yatasaidia sana kundi hili la bodaboda.,
Ameongeza kuwa Ajali za barabarani zinsababisha hasara kubwa kwa taifa, familia na jamii kwa ujumla. Hasara hizi ni Pamoja na kupoteza wapendwa wetu ambao wengine tunawategemea, ulemavu wa kudumu pamoja na gharama kubwa za matibabu kwa wahanga wa ajli. Kwa Pamoja tukiungana tunaweza kupunguza sana kama siyo kumaliza kabisa tatizo hili.
Mwakilishi wa waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam Boniface Mtale alisema ajali za bodaboda zimekuwa zikiongezeka kwa kasi na kufafanua kuwa uelewa mdogo wa sheria na kanuni za usalama barabarani zimekuwa ndiyo chanzo kikuu cha ajali hizo.
“Uelewa mdogo wa sheria na kanuni za usalama barabarabi bado ni changamoto kubwa kwa madereva wengi wa bodaboda. Tunawashukuru sana BetPawa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kutambua tatizo hili na kuamua kutupatia elimu hii muhimu sana kwetu,” alisema
#KonceptTVUpdates