Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mkazi wa Mbalizi, Maloki Mwaihoyo (75) kwa tuhuma za kumuua mjukuu wake Vission Nyaliko mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kwa kumkata na jembe wakati akichimba udongo.
Kamanda wa Jeshi hilo, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea Alhamisi Agosti 31 huko Tarafa ya Tembela Wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo mtuhumiwa ambaye ana uoni hafifu alikuwa akichimba udongo kwa ajili ya kukandika nyumba yake.
Aidha kamanda Kuzaga amewasihi wazazi wenye Watoto wachanga kutowaachia wazazi wasio na uwezo wa kuwalea Watoto hao ili kuepusha vifo Pamoja na madhara kama hayo.
#KonceptTVUpdates