Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu Leo Septemba 6,2023 amesitisha shughuli za Bunge kwa saa Moja kisha Wabunge wote warejee tena Ndani ya Ukumbi wa Bunge ili waendelee na shughuli za Bunge.
Naibu Spika Zungu amesitisha shughuli hizo za Bunge kwa mamlaka aliyokuwa nayo chini ya kanuni 97 fasiri ndogo Moja ya kanuni za Kudumu za Bunge toleo la februari 2023 ambapo ameielekeza kamati ya utawala wa katiba na Sheria kwenda kufanyia kazi muswada wa Sheria wa marekebisho wa Sheria mbalimbali namba 3 wa mwaka 2023 ambao tayari umeshasomwa Bungeni.
#KonceptTVUpdates