ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, October 3, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

DKT. BITEKO ”TANESCO WATANZANIA WANATAKA UMEME”

SUZO SHUKRANI by SUZO SHUKRANI
Sep 14, 2023
in HABARI
0
DKT. BITEKO ”TANESCO WATANZANIA WANATAKA UMEME”
0
SHARES
18
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

Oct 2, 2023

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

Oct 2, 2023

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

Oct 2, 2023
Load More

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema watanzania wanataka umeme na hivyo kuwataka Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kufanya kila jitihada za kuhakikisha kunakuwa na nishati ya uhakika.

Ameyasema hayo Septemba 13, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika hilo na kuongeza kuwa zinahitajika jitihada za dhati za kuhakikisha kunakuwa na rasilimali watu ya kutosha pamoja na mahusiano mazuri kazini hatua ambayo itaboresha utendaji kazi wa shirika hilo.

“Watanzania wanataka umeme, hata tungekuwa na mipango ya namna gani watanzania wanachotaka ni umeme, unaweza kusema fulani anafanya hivi, au mchakato wa kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kunua kifaa fulani unaenda hivi lakini watanzania hayo hawayajui, wao wanamjua TANESCO ndio mleta umeme, katika kazi zetu na Taasisi nyingine za Serikali moja ya mambo tunayotakiwa kufanya ni kuziungaunisha taasisi nyingine ili tuweze kuwafikia watanzania kwa haraka, na kazi hii ni ya kwetu” amesema Dkt. Biteko.

Amewataka Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kushughulikia mambo badala ya kushughulika na watu hali ambayo ameitaja kuwa inavunja ari ya kufanya kazi.

”Kama viongozi mtawagawanya wafanyakazi kwenye makundi, mahali pa kazi patakuwa pagumu kwa sababu mtakuwa mmekusanya genge la soga na wapiga majungu kazini, na mwisho watanzania hawatapata umeme, wafanyeni watu hawa kuwa ni daraja linalofanana na kama tutashughulika na masuala binafsi ya watu badala ya masuala ya kazi hatutafikia malengo, kuna watu wanahofu ya mabadiliko, na hali hiyo tunaitengeneza sisi viongozi, kwa sababu ukiingia mahali badala ya kushughulika na jambo unaanza kushughulika na watu, na wafanyakazi wote hawa maisha yao yote ya utumishi wao masaa mengi wanatumia wakiwa kazini, hawa ni binaadamu, kuna wakati watakuwa wamekwazwa, wamevunjika moyo. Mahali wanapofanyia kazi kuwe ni kimbilio kwao.” amesema Dkt. Biteko.

 

#KonceptTVUpdates

Related

SUZO SHUKRANI

SUZO SHUKRANI

Related Posts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10
HABARI

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
HABARI

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM
HABARI

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI
BIASHARA

MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA
HABARI

SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA
HABARI

TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

September 2023
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Aug   Oct »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In