ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, October 3, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

DKT. MPANGO TANZANIA ITAENDELEA KUTOA MCHANGO IFAD

SUZO SHUKRANI by SUZO SHUKRANI
Sep 6, 2023
in HABARI
0
DKT. MPANGO TANZANIA ITAENDELEA KUTOA MCHANGO IFAD
0
SHARES
23
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 06 Septemba 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Geraldine Mukeshimana. Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

RelatedPosts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

Oct 2, 2023

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

Oct 2, 2023

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

Oct 2, 2023
Load More

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema Tanzania itaendelea kutoa mchango wake katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ili kuwezesha utekelezaji mbalimbali wa miradi unaofanywa na mfuko huo. Amesema mageuzi katika sekta ya kilimo ni kipaumbele cha serikali ya Tanzania kwa kuwa inatambua umuhimu wake katika uchumi wa nchi.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa IFAD kuona umuhimu wa kuongeza eneo la mradi wa urejelezaji ardhi katika maeneo yanayokabiliwa na ukame Tanzania bara na Zanzibar. Pia amesisitiza umuhimu wa kuzingatia mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji kulingana na uwekezaji halisi wa miradi ili iweze kutekelezwa kwa wakati.

Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa IFAD kushirikiana na Tanzania katika tafiti za kina zitakazowezesha matumizi ya ardhi katika maeneo yenye ukame husasani maeneo ya kanda ya kati ya nchi ili iweze kutumika katika kilimo. Pia amesema ni muhimu kuweka mkazo katika miradi itakayowezesha matumizi sahihi ya rasilimali za majini kama vile baharini na katika maziwa ili kwenda sambamba na vipaumbele vya nchi katika sekta ya uchumi wa buluu.

Kwa Upande wake Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Geraldine Mukeshimana amesema Tanzania imekuwa ni mdau muhimu katika mfuko huo kwa kuwa mchangiaji mzuri na hivyo kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Amesema kutokana na athari za migogoro ya kimataifa na uviko 19 iliyosababisha ukosefu wa chakula katika maeneo mengi, IFAD inalenga kuhamasisha uchangiaji wa rasilimali fedha kutoka kwa nchi washirika ili iweze kutoa mchango wake katika kuimarisha sekta ya kilimo.

 

 

#KonceptTVUpdates

Related

SUZO SHUKRANI

SUZO SHUKRANI

Related Posts

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10
HABARI

KANISA LAPOROMOKA MEXICO NA KUUWA WATU 10

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
HABARI

TAKRIBAN WAHAMIAJI 10 WAMEFARIKI NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA LORI NCHINI MEXICO

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM
HABARI

AIRPORT YA ZANZIBAR IPO BUSY KULIKO YA DAR ES SALAAM

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI
BIASHARA

MIFUMO YA KIFEDHA KULINDWA ZAIDI

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA
HABARI

SIKU 7 ZATOLEWA MILANGO KUBADILISHWA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023
TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA
HABARI

TWENDE BUTIAMA YAANZA RASMI KUTOKA DAR MPAKA BUTIAMA

by SUZO SHUKRANI
Oct 2, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

September 2023
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Aug   Oct »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In